Wajawazito Selela Wajifungua kwa Tochi za Simu

Ferdinand Shayo,Arusha. Wajawazito katika zahanati ya kijiji cha Selela kata ya Selela wilaya ya Monduli mkoani Arusha wamelazimika kujifungua kwa kutumia tochi za simu pamoja na taa ya chemli kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme kwa takribani mwezi mmoja na wiki mbili. Kinamama wa kijiji hicho Tumaini Shirima na Mwasiti Hemedy wameeleza kuwa wamekua wakiwapeleka wajawazito kwenye zahanati hiyo …

Serikali Kuanzisha Utendaji wa Mikataba kwa Watumishi Wake

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO – Dar es Salaam Serikali imejipanga kuanzisha mikataba ya utendaji kazi kwa Taasisi za Umma katika mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya kuhakikisha watumishi hawafanyi kazi kwa mazoea. Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki …

Msanii wa Nigeria Alhaji Akisaidia Kituo cha Yatima Kigamboni

    Na Sheila Simba, Maelezo MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shillingi milioni 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Kigamboni Community Center(KCC). Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa …

Waziri Awataka Watumishi wa Umma Kutambua Haki Zao

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amewasisitiza watumishi wa Umma kufahamu kanuni za kudumu za utumishi wa umma ili kutambua haki zao na kuepuka kunyanyaswa na waajiri wao. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri huyo alipokuwa akiongea na mwandishi …

Mkwasa Abadili Kikosi Cha Taifa Stars

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles. Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa …

Mechi ya Yanga na JKT Ruvu Yapigwa Kalenda

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imethibitisha kuwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na JKT Ruvu ya Pwani, ulipangwa kufanyika Jumatano Agosti 31, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeahirishwa mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine. Mechi hiyo imeondolewa kutokana na timu ya Young …