Kivuko cha Mv. Magogoni KIVUKO cha MV. Magogoni kimepokelewa na kuanza kazi rasmi ya kutoa huduma za usafirishaji kati ya eneo la Kigamboni na Magogoni mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa. Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kukipokea kivuko hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema …
Rais Dk Magufuli Amwaga Neema kwa Waliokuwa Wakazi Nyumba za Magomeni Kota
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika nyumba za Magomeni Kota ambazo zilivunjwa kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi na Biashara ambao walitelekekezwa kwa muda mrefu na manispaa ya Kinondoni na kuwafanya waishi maisha magumu. Katika hotuba yake Rais ameahidi kuwajengea nyumba za kisasa wakazi hao 644 ambapo wataishi …
Waziri Muhongo Kuwapa Ruzuku Wachimbaji Madini Wadogo
Na Daudi Manongi, MAELEZO-Dar es Salaam SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati na Madini imepanga kuwapatia ruzuku wachimbaji wadogo wa madini ili kuongeza mchango wa madini katika pato la taifa kutoka asilimia 3.5 ya sasa hadi 10. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha Tunatekeleza kinachorushwa na kituo cha …
UNESCO Yatenga Zaidi ya Bilioni 3 Kuwasaidia Watoto wa Kike…!
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Maimuna Tarishi akizungumza kuhusu mipango ya serikali kukabiliana na tatizo la watoto wa kike kukatishwa masomo. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Hashina Begum akizungumzia sababu ya watoto wa kike kutokuwepo shuleni na jinsi ambavyo UNWOMEN watashiriki katika mradi wa kusaidia watoto wa kike kurudi shuleni. …
Shangwe Uganda Kufurahia Kufuzu AFCON 2017
Sherehe zimekuwa zikiendelea kote nchini Uganda kufuatia timu ya taifa ya nchi hiyo kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika baada ya kusubiri kwa kipindi cha karibu miaka 40. Mara ya mwisho Uganda ilicheza Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1978. Wamefuzu tena baada ya kuishinda Comoro 1-0 mjini Kampala.Omar Mutasa alikuwepo na ana maelezo zaidi.