Wafanyabiashara Kukutana Kongo Kujadili Changamoto

  Na Lilian Lundo – MAELEZO ZAIDI ya wafanyabiashara 100 kutoka Tanzania na Kongo wanatarajia kushiriki kongamano la biashara litakalofanyika Lubumbashi Kongo Septemba 22 mwaka huu. Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuongeza kiasi cha mauzo ya nje na kuboreshwa mazingira mazuri ya biashara kati ya nchi hizo mbili. “Wafanyabiashara wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kupata …

Upangaji Bora Matumizi Ardhi Utapunguza Migogoro ya Ardhi-RC Moro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Kebwe akipongeza hatua ya upimaji wa ardhi na kuahidi kuendelea kutembelea kuona maendeleo. Bw. Ally Amri(kushoto) ambaye ni  Land Surveyor akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Kebwe namna zoezi la upimaji linavyofanyika.  Christian Thomas (aliyevaa shati la blue) ambaye ni mwenyekiti wa kijiji akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Kebwe namna …

Unajua Madhara ya fluoride ya Kwenye Dawa ya Mswaki

Tafadhari soma hii ili uangalie madhara yanayopatikana kupitia #FLUORIDE inayowekwa kwenye dawa za meno, Kwa kuthibitisha hili kasome box la dawa ya meno unayotumia yenye fluoride utakuta wameandika #usimeze na mtoto chini ya miaka sita apige mswaki chini ya uangalizi wa mzazi na hata ukipiga ukiswaki basi sukutua sana kiusahihi na kiumakini, kwa sababu Fluoride ni moja kati ya madawa …

Prof. Mbarawa Atoa Miezi Sita Upanuzi Uwanja wa Ndege Mwanza

    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja huo ifikapo mwezi Februari Mwakani. Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la watembea …

Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi Salama – Kamanda Mpinga

  Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limetangaza tarehe ya kuanza kwa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo mwaka huu inatarajia kufanyika kitaifa Mkoani Geita. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, DCP Mohamed Mpinga alisema maadhimisho ya mwaka huu yamepewa kauli …

Mkuu wa Wilaya Awapongeza Wamasai Kuacha Mila Potofu

Na Mathias Canal, Kilimanjaro MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule amewapongeza baadhi ya vijana wa kimasai kwa kuachana na imani potofu na hatimaye kuanza kumwabudu Mungu kwa kuhudhuria Misa mbalimbali katika makanisa. Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo wakati wa sherehe maalumu kwa waliokuwa vijana wa Kimasai (Morani) kuingia hatua kubwa ya uzeeni …