Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita (kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya mtaa huo iliyofanyika Hoteli ya Best Western Plus Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta. Mkutano na wanahabari ukiendelea kabla ya uzinduzi huo. Wajumbe …
Waziri Jenista Mhagama Ataka Misaada Waathirika wa Tetemeko Kusimamiwa
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amewataka Viongozi wa Serikali mkoani Kagera kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi ya vifaa vya misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea hivi karibuni mkoani humo. Waziri Jenista aliyasema hayo leo wakati alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kukagua taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo shule za msingi ileega …
Bodi ya Magazeti ya CCM Yajiuzulu…!
BODI ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavyo ni Uhuru Publications Limited (UPL) wachapishaji wa Gazeti la Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Peoples’ Media Communication Limited (PMCL) inayoendesha kituo cha redio Uhuru imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Al-haj Adam O. Kimbisa. Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi na …
Waziri Awataka Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi Kuungana
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kuungana ili waweze kupata fursa katika miradi mikubwa ya ujenzi itakayoanza hivi karibuni hapa nchini. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina endelevu ya 26 ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Prof. Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ujenzi …
Klabu ya Simba Kutumia Mawakala Kuuza Bidhaa Mikoani
Katika kupanua wigo wake wa kibiashara lakini pia katika kuwafikishia wanachama, wapenzi na mashabiki wake, Klabu ya Simba imeanzisha mpango maalumu wa kutafuta mawakala ambao watatambuliwa na klabu ya Simba ili kuweza kuuza bidhaa zake mbalimbali sehemu zote za Tanzania. Katika kulifanikisha hilo Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG Group Imani Kajula, ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala …
Sekondari Kongwa Zapangiwa Wastani wa Ufaulu…!
Na Mathias Canal, Dodoma MKUU wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka. Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo …