RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe Taarifa iliyotolewa leo tarehe …
Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi Wamtembelea Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi Profesa Ruth Meena ambaye pamoja na ujumbe wake uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza naye Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Mtandao …
NEC Yawataka Wanafunzi Sekondari Kuwa Mabalozi Elimu ya Mpiga Kura
Na Aron Msigwa – NEC, Bariadi TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wanafunzi wa shule za Sekondari waliopatiwa elimu ya Mpiga Kura katika maeneo mbalimbali nchini kuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu waliyoipata kwa jamii inayowazunguka. Wito huo umetolewa na Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Fausta Mahenge wakati akitoa elimu ya mpiga …
Profesa Mbarawa Awabana Madereva wa Malori ya Mchanga na Kokoto
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wa malori ya mchanga na kokoto watakaobainika kutofuata sheria za ubebaji wa bidhaa hiyo na hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara. Waziri Mbarawa …
Ujerumani Wajenga Jumba la Mwalimu Nyerere, AU
KANSELA wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la Rais wa Kwanza wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere. Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka nchini Ujerumani. Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU …