Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Yawanoa Wanahabari

  Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza, wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.  Pia wanahabari hao walipata wasaa wa kuwasilisha tathimini yao kuhusiana na ziara mbalimbali ambao wamezifanya kwenye maeneo yenye wawekezaji wa madini Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo …

Vijana Watakiwa Kuwa Wabunifu na Wasaka Fursa

KUFUATIA changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika …

Kichuya Abeba Mpunga wa Mwezi

Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017. Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC. Mchezaji aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo …

Azam, Mtibwa Vitani Leo Taifa

Michezo sita itafanyika leo Jumatano Oktoba 19, mwaka huu wakati keshokutwa Alhamisi Oktoba 20, kutakuwa na mchezo mmoja tu. Mchezo wa leo Na. 86 wa VPL utafanyika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani kabla ya kesho Oktoba 19, mwaka huu kuendelea kwa mechi sita pia za mzunguko 11 wa kukamilisha raundi ya kwanza kwa msimu 2016/17. Kampuni hizo zinazong’arisha VPL, kesho …

Acha Kuchezea Moto wa Leicester City

Klabu ya soka ya Leicester City imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya ligi binya magwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Copenhagen. Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani King Power, Leicester walipata bao hilo dakika tano kabla ya kwenda mapumzikoni kupitia kwa Riyad Mahrez aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu baada …

Namaingo Kunufaisha Wananchi 3,000 Ufugaji Kuku Mkoani Lindi

      KAMPUNI ya Namaingo Business Agency (T) LTD, mwezi ujao inazindua mradi mkubwa wa ufugaji kuku chotara wenye thamani ya sh. bilioni 30 utakaowawezesha wananchi 3000 wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ubwa Ibrahim  amesema …