Trump Asema Clinton Atareta Vita ya Dunia Utatua Mzozo Syria

MGOMBEA nafasi ya urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican, Donald Trump amesema mpango wa mpinzani wake Hillary Clinton kuhusu kutatua mzozo Syria utaanzisha “Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia”. Alisema Marekani inafaa kuangazia zaidi kushinda vita dhidi ya kundi linalojiita Islamic State badala ya kulenga kumshawishi au kumshinikiza Rais wa Syria Bashar al-Assad kung’atuka uongozini. Bi Clinton amekuwa akipendekeza …

Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa Tanzania

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi akifungua rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima. Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wenye …

Arsena, Liverpool Wazidi Kusonga Mbele EFL

Arsenal wameendeleza rekodi yao ya kutoshindwa hadi mechi 14 baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kuwafungia mabao mawili na kuwawezesha kuondoka na ushindi dhidi ya Reading katika Kombe la EFL. Kiungo huyo wa kati wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 33.Reading karibu wasawazishe baada ya mpira wakupinduliwa, wake Callum Harriott kutua juu ya lango lililokuwa linalindwa na Emiliano Martinez. Arsenal …

Kifo cha Carlos Alberto Chaacha Maswali Mengi

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72. Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali. Beki wa kulia …

Serikali Itaendelea Kudumisha Uhusiano na Ushirikiano Kati ya Tanzania na India

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na India ambayo yamedumu kwa muda mrefu hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo za elimu,afya na biashara. Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo 25-Oct-2016 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Sandeep Arya Ikulu …

Wafanyakazi wa NMB Mandela Watoa Msaada kwa Wagonjwa Hospitali ya Rufaa Mawenzi

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakishusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi. Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha akimueleza jambo Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitai ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface walipofika hospitalini hapo kutoa zawadi …