KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL. Kampeni hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W. Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi wa …
Donald Trump Aibuka Kidedea, Obama Amwalika Ikulu…!
DONALD Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali. Bi. Clinton amempigia simu Bw. Trump kumpongeza kwa ushindi wake. Rais Obama pia amempigia simu kumpongeza na kutangaza kwamba amemwalika Ikulu ya White House siku ya Alhamisi washauriane kuhusu shughuli ya mpito. Bw Trump, aliyeeleza nia yake ya kuwafanyia kazi Wamarekani wote atakapoingia madarakani, …
Jaji Mutungi Avifuta APPT Maendeleo, Jahazi Asilia na Chausta
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Msajili wa Vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi. Mkutano na wanahabari ukiendelea. Na Dotto Mwaibale …
CCM Watuma Rambirambi Kifo cha Joseph Mungai
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg. Jesca Msambatavangu kufuatia kifo cha Mhe Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi kilichotokea jana tarehe 08 Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Mhe. Mungai, ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na …
Nape Nnauye ‘Awapasha’ Wadau wa Michezo
Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa wadau wamichezo nchini kuacha kukimbilia Mahakamani wanapokuwa na migogoro bali watumie vyombo vya kusimamia michezo kutafuta suluhu. Wito ameutoa leo jijini Dar es Salaam alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu kupata taarifa ya mgogoro wa Chama cha Riadha …
Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli: PPF Watekeleza kwa Vitendo…!
Na Daudi Manongi, MAELEZO. NOVEMBA 5 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani akiwa na dhamira mpya ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa akisisitiza umuhimu wa viwanda …