Duru la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu. Katika mechi za kesho, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa …
Oscar Kuwapiku Mesi, Ronaldo Kimpunga
Mchezaji wa Chelsea Oscar anatarajiwa kuwa mchezaji soka anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani atakapohamia Ligi Kuu ya Uchina mwezi Januari. Shanghai SIPG wanatarajiwa kulipa £60m kumchukua kiungo huyo wa kati kutoka Brazil. Akifanikiwa kuondoka, basi Oscar, 25, ataungana na meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ndiye mkufunzi wa Shanghai. Taarifa zinasema atakuwa analipwa £400,000 kila wiki …
Prof. Mgaya Ateuliwa Kuwa Mkurugenzi Mkuu NIMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Desemba, 2016 amemteua Prof. Yunus D. Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Uteuzi wa Prof. Yunus D. Mgaya unaanza mara moja. Prof. Yunus D. Mgaya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Mwele Malecela ambaye uteuzi wake umetenguliwa. …
Namaingo Business Agency Kukabidhi Sungura kwa Wajasiliamali 2000
KAMPUNI ya Namaingo, kugawa sungura 600 kwa Wajasiriamali 2000 Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa nchini. Mpango huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari eneo la mradi huo wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam jana. Alisema kuwa walengwa watakaonufaika na mradi huo, …
Bwana Harusi Aingia Mitini Muda Mfupi Kabla ya Ndoa…!
UNAWEZA kusema kuwa mwisho wa mwaka 2016 huenda na matukio ya vioja. Kimetokea kituko cha aina yake katika Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa wa Mbeya mara baada ya bwanaharusi kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa. Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini. Imeelezwa kuwa mipango …
Matukio Mahafali ya Pili Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Prof Faustine Bee akimuongoza Mkuu wa Chuo hicho Pius Msekwa wakati akiwasili katika uwanja wa Chuo hicho kwa ajili ya Mahafali ya Pili. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Prof Gerald Monela akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa …