TTCL YAZINDUWA HUDUMA YA 4G LTE MKOANI MWANZA
KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, imezindua Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza siku ya Jumatatu, Januari 23, 2017. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela alieongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Mary Tesha Onesmo na Kamanda wa Polisi Mkoa …
Kamati ya Taifa Matumizi ya Bioteknolojia Salama Yaridhika na Utafiti wa Mahindi…!
Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wajumbe wa NBC katika kituo hicho cha utafiti wa kilimo cha Makutupora cha mkoani Dodoma. Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kkushoto), akitoa maelezo mafupi kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kabla …
AU Kujadili Madai ya Haki za Ardhi kwa Wanawake Barani Afrika
Meneja wa Haki za Wanawake kutoka Actionaid Tanzania, Scholastica Haule akionesha nakala yenye madai hayo kwa vyombo vya habari walipokutana kumpongeza Mjumbe mwakilishi kutoka nchi za Afrika Mashariki wa Baraza la Wanawake wa Vijijini, Florah Mathias kupata nafasi hiyo.
Rais Donald Trump Aanza Kuzibadili Sheria za Obama
RAIS wa Marekani Donald Trump ameanza kutia saini maagizo ya rais, baadhi yake yakiwa ni ya kubadili yale yalioafikiwa na mtangulizi wake Barak Obama. Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake, Bw Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obamacare, ambayo …
Watakiwa Kujitokeza Kuchagua Madiwani, Mbunge
Na Aron Msigwa –NEC, Zanzibar TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata 19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani kwa upande Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3. Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume …