Namaingo Watakiwa Kuchangamkia Uzalishaji wa Malighafi za Viwanda

Na Richard Mwaikenda SERIKALI imeutaka Ushirika wa Vibidar Namaingo kuanza kuzalisha mazao mengi kwa ajili ya malighafi ya viwanda vilivyopo na vinavyotarajiwa kuanzishwa nchini. Ushauri huo ulitolewa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo wakati wa sherehe ya kukabidhi cheti kwa ushirika huo wa Vikundi vya Biashara Dar es Salaam (Vibidar), kwenye Uwanja wa …

CCM Yatuma Rambirambi Ajali Iliyouwa Saba Kilimanjaro

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa …

Mti wa Kihistoria Waanguka Makumbusho ya Taifa Dar

  MTI mkubwa wa kihistoria aina ya Mkuyu wenye kusadikiwa na miaka zaidi ya mia moja (100) uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam umekatika tawi kubwa na kuangukia sehemu ya jumba hilo na kuleta madhara kidogo kwenye Jengo hilo. Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea mnamo saa saba mchana walisema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha mara …

Waliosusia Maiti ya Kichanga Amana Wamtaka Waziri wa Afya…!

Na Dotto Mwaibale SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake huku akidai kabadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana, Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio …