
Baadhi ya Vijana walioachana na madawa ya kulevya Soba House No 1 Wete Pemba wakimskiliza Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Bi. Jokha Khamis Makame, (hayupo pichani) alipozungumza nao kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein, baada ya kuwakabidhi vyakula alipofanya ziara maalum ya kuwatembelea.

Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Bi. Jokha Khamis Makame, kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi vyakula
msaidizi katibu wa Soba House iliyopo Mkanjuni wilaya ya Chake chake, vyakula vikiwemo Unga ngano, Mchele Mafuta na Tende na Mafuta ya kupikia, kwa ajili ya vijana walioachana na madawa ya kulevya.[Picha na Ramadhan Othman, Pemba.]