Kenyatta Awafukuza Kazi Mawaziri, Aunda Upya Wizara

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kufuatia shinikizo la Wananchi kudai kwamba kuna idadi kubwa ya mawaziri wake wanatuhumiwa na ufisadi.

Kwa mujibu wa taarifa zaidi zinasema katika baraza hilo la mawaziri limeongezwa wizara moja huku akiwapiga chini mawaziri sita wanaokabiliwa na kashfa za ufisadi.

Katika mabadiliko hayo Kenyatta kwa sasa atakuwa na jumla ya wizara 20 huku akiwa na mawaziri wanne wanawake wanaounda baraza hilo.
-BBC