Israel Yaweka Kamera za Ulinzi eneo Takatifu Jerusalem

Vikosi vya Israel

 

ISRAEL imeweka kamera eneo la kuingilia katika uzio wa Msikiti wa Al-Aqsa katika Mji mkongwe wa Jeruslem. Hatua hiyo imechukuliea wakati mvutano mkubwa kuhusiana na hatua za usalama kwenye eneo hilo, ambalo waislamu wanaliita Haram Al-Sharif na wayahudi wanaita Temple Mount.

Waumini wa Palestina wamepinga vikali Israil kuweka mitambo ya kun’gamua kama mtu amebeba kitu cha chuma, baada ya askari polisi wawili wa Israil kuuwawa. Wapalestina watatu waliuawa wakati wa ghasia na vikosi vya Israel siku ya Ijumaa, wakati maelfu waliandamana mashariki mwa Jerusalem na eneo la linalomilikiwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.

Baadaye raia watatu wa Israel wakauawa kwa kuchomwa visu katika makao ya walowezi wa kiyahudi karibu na Ramallah na mshambuliaji mpalestina ambaye aliingia nyumbani kwao.
-BBC