Raila Odinga ‘aitisha’ mgomo wa wafuasi kupinga matokeo ya uchaguzi

Wafuasi wa upinzani wakiandana mtaa wa Mathare Nairobi

KINARA wa muungano upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amewashauri wafuasi wake kususia kazi siku ya Jumatatu kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyikia Jumanne iliyopita. Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga amedai kuwa serikali ilikiwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani kabla ya kutangazwa matokeo.

Aidha Odinga amesema kuwa siku ya Jumanne, mrengo wa Nasa utatangaza mwelekeo ambao utachukua. Rais Uhuru Kenyatta alitangzwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raia Odinga akipata kura 6,762,224.