TFF Yawakumbuka Mashabiki Kwa Sapoti Yao

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewapongeza viongozi, mashabiki, wachezaji wa vilabu na timu za Taifa kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya kimataifa iliyochezwa mpaka sasa. Katika kipindi cha mwezi mmoja, Tanzania imeshiriki katika michuano mbalimbali ya kirafiki, mashindano ngazi za vilabu, timu za taifa ikiwemo ya Wanawake (Twiga Stars), Vijana (Serengeti Boys) na Taifa Stars. Katika michezo …

Manchester City Waing’oa PSG, Ronaldo Apiga Hattrick UEFA

Timu ya soka ya Manchester city imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya baada ya kuwafunga PSG ya Ufaransa jumla ya bao 1-0. Wakicheza katika dimba lao la Etihad Manchester city walifanikiwa kuandika bao pekee na la ushindi Dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji De Bruyne. Kwa ushindi huo …

Soma Hapa Ratiba ya Kombe la Shirikisho

Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imefanyika usiku wa jana huu moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo, huku timu za Coastal Union na Mwadui FC zikipata nafasi ya kucheza nyumbani. Katika droo hiyo iliyochezeshwa na mchezaji mstaafu wa timu ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Esther Chaburuma, imewashuhudia …

Rais Kenyatta Aahidi Kutimiza Matakwa ya WADA

Kenya itatimiza muda wa mwisho wa mwezi Mei kufuata mfumo wa shirika linalopambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu misuli, WADA na kuepuka vikwazo Vikwazo hivyo ni pamoja na kupigwa marufuku kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya Rio. Akizungumza katika hafla ya chai ya asubuhi aliyowaandalia wanariadha watakaoshiriki katika mbio ndefu, marathon na mbio za dunia za nusu marathon …

Wasii wa Filamu Kuigiza Filamu Katika Hifadhi za Taifa

Wasanii wa Filamu nchini kote wametakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika maeneo ya hifadhi za taifa kwenye shughuli zao za kurekodi filamu badala ya kutumia majengo ya kifahari ili kutangaza utalii kwa kupitia kazi zao. Hayo yameelezwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA ,Pascal Shelutete wakati akizungumza katika Tamasha la Chama Wasanii wa filamu jijini …

Biashara ya Simba Kwishaaaaaaaaaaaa

Hatua ya Robo fainali ya mwisho ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (Federation Cup) imepigwa jana kati ya Coastal Union dhidi ya Simba katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na huku coastal Union ikifanikiwa kuitoa Simba katika michuano hiyo kwa ushindi wa Bao 2-1. Magoli ya coastal yamefungwa na Mchezaji wa Cameroon Youssouf Sabo,huku goli la Simba …