Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza. Katika salamu zake, TFF imewapa pole familia ya marehemu Ngofilo ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu …
Matokeo na Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza Soma Hapa
Klabu ya Manchester United wameweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nne bora Ligi ya Uingereza kwa kulaza Aston Villa 1-0 uwanjani Old Trafford. Bao la United lilifungwa na chipukizi Marcus Rashford. Matokeo hayo hata hivyo yana maana kwamba Aston Villa wameshushwa daraja. Villa wanashika mkia wakiwa na alama 16 baada ya kucheza mechi 34. Newcastle United, walio hatarini ya …
Yanga Waleeee Wanaonekana Kwa Tochi
Timu ya Yanga imefanikiwa kurejea kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuifunga mtibwa Sugar kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa leo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa. Bao pekee la ushindi limefungwa na Simon Msuva dakika ya 48 kipindi cha pili kwa kiki ya chinichini aliyoiachia akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda mlinda mlango wa …
Rais waSoka Ujerumani Apewa Jukumu la Kurejesha Uaminifu
Reinhard Grindel amechaguliwa kuwa rais wa Shirikisho la Kandanda la Ujerumani – DFB, na kupewa jukumu la kurejesha uaminifu kufuatia kashfa iliyotokana na malipo ya kutatanisha kabla ya Kombe la Dunia la 2006 Grindel mwenye umri wa miaka 54, alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo. Anachukua nafasi ya Wolfgang Niersbach, aliyejiuzulu mwezi Novemba wakati kashfa hiyo ilianza kufichuka. Grindel, mwanasiasa …
Kipute cha Ligi Kuu Bongo Kuendelea Tena Kesho
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi. Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar …
Rais wa TFF Jamal Malinzi Amwaga Pongezi kwa Ravia
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba. Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA katika kipindi kingine. Malinzi amewapongeza …