Kichuya wa Mtibwa Awa Mchezaji Bora wa Mwezi

Mshambuliaji Shiza Ramadhan Kichuya wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2015/2016. Kichuya alionyesha kiwango cha juu katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, hivyo kuisaidia timu yake kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza. Katika mechi hizo ambazo zote Kichuya alicheza, alifanikiwa kufunga mabao …

Malinzi Atuma Salamu za Pongezi Ujerumani

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametumia salamu za pongezi, Reinhard Grindel kwa kuchaguliwa rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ujerumani (DFB). Katika salamu zake kwenda DFB, Malinzi amempongeza Grindel kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi ambao hakuwa na mpinzani, na kusema hiyo imeonyesha imani ya watu wa Ujerumani dhidi yake …

Mashabiki Wasimba Wawekwa Kikaangoni

Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana …

Siku za Hazard Ndani ya Chelsea Zinahesabika

Kocha wa kikosi cha Chelsea Guus Hiddink amesema kiungo wa timu hiyo Eden Hazard yuko kizani msimu huu. Katika msimu huu kiungo huyu amefunga mabao mawili tu katika michuano ya kombe la Fa huku akiwa hajazifumania nyavu katika michezo ya ligi kuu. Hazard,mwenye umri wa miaka 25, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa (PFA) Mwaka 2015. Kiungo huyu amebakiza …

Arsenal, Lecester City Mambao Yazidi Kuwa Magum

Klabu ya Arsenal imezidi Kuboteza matumaini ya kunyakua taji la ligi kuu la uingereza baada ya kulazimishwa sare na timu ya Crystal Palace ya Bao 1-1 bao la arsenal lilfngwa dakika 45′ na Sanchez huku lile la Crystal lilifungwa dakika ya 82 na Yannick Bolasie Matokeo Mengine AFC Bournemouth 1:2 Liverpool Leicester City 2:2 West Ham United Arsenal 1:1 Crystal …

Toto Yaharibu Hesabu za Simba Taifa

Klabu ya Simba imefungwa bao 1-0 na Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waziri Junior ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 20 kwa shuti kali la umbali wa mita 20 lililomshinda kipa Muivory Coast, Vincent Angban. Simba inayobaki na pointi zake 57 baada …