Azam Yaaga Michuano Baada ya Kukubali Kichapo

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia. Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la …

Serengeti Boys Kutimkia Nchini India

Timu ya taifa ya Tanzania vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kushiriki mashindano maalumu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini India, yatakayozishirikisha nchi za Marekani, Malasyia na Korea Kusini na wenyeji mapema mwezi Mei, 2016. Chama cha Soka nchini India (AIFF) kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni …

TFF Yaweka Mkono wa Baraka kwa Yanga na Azam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF). TFF imezitaka Azam FC na Yanga kupambana katika michezo yao ugenini ili kupata matokeo mazuri yatakayozifanya ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, ikiwa kwa sasa ndio wawakilishi …

TP Mazembe Wakabiliwa na Kibarua Kigumu

klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika jitihada zake za kutetea taji lao. Mazembe wanahitaji kuwafunga Wydad kwa zaidi ya mabao mawili kwa bila ili kunusuru hadhi yao baada ya kuchapwa 2-0 katika mchezo wa kwanza Juma lililopita . Leo Alex McLeish ataiongoza Zamalek ya Misri …

Vardy Kitanzini Kwa Kumkaripia Mwamuzi

Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu na chama cha soka cha nchini England FA. Vardy alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu baada ya kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Jon Moss katika mchezo wa Jumapili dhidi ya West Ham. Ripoti ya mwamuzi huyo imedai kuwa mshambuliaji huyo alifanya utovu wa nidhamu kwa majibu yake mara …

Spurs Yashinda Nne Mtungi, Leicester City Wahaha

Klabu ya soka ya Tottenham wakicheza ugenini katika dimba la Brittania wameibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City. Mshambuliaji mahiri wa kikosi cha Spurs Harry Kane alianza kuzifumania nyavu katika dakika ya tisa ya mchezo, kisha kiungo Delle Ali akaongeza bao la pili katika dakika ya 67 kipindi cha pili. Katika dakika ya 71 Harry …