Wakicheza Ugenini huko Nchini Misri, Yanga wamefungwa 2-1 na Al Ahly na kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa Africa. Mabingwa watetezi Tp Mazembe wakaondolewa katika michuano hiyo baada ya sare ya 1-1 dhidi Wydad de Casablanca, na Casablanca wakisonga mbele kwa ushindi 3-1. Enyimba wakasonga mbele kwa ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Etoile du Sahel ,As Vita Club nao …
Rais wa ZFA Apokea Salamu za Pongezi Kutoka kwa Hayatou
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika. Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar …
Machester City Yapanwa Mbavu na Newcastle
Klabu ya Mnchester City Imeambulia Sare ya Bao 1-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St James’ Park usiku wa Jana Jumanne. Bao la Man City lilifungwa na Sergio Aguero dakika ya 14, kabla ya Vurnon Anita kuiswazishia Newcastle dakika ya 60 Ratiba ya Leo 20 April West Ham v. Watford Liverpool v. …
Nahodha wa Azam Asema Nguvu Zote Zinahamia FA
NAHODHA Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao, amewafuta machozi wote wa timu hiyo baada ya kutolewa jana na Esperance ya Tunisia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Himid aliyeingia dakika ya 79 katika mtanange huo kuchukua nafasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amewaambia mashabiki hao kuwa kwa sasa nguvu zao zote wanahamishia katika Ligi …
Balotelli Agoma Kurudi Liverpool
Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli amesema hataki kurejea klabu yake ya Liverpool baada ya kipindi chake cha mkopo klabu ya AC Milan kumalizika mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na klabu hiyo yake ya zamani Agosti kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Anfield. Balotelli amehangaika na amefunga mabao matatu pekee katika mechi 19 alizocheza. …
Yanga Kuweka Historia Mpya Misri Leo?
Watanzania wengi leo yanaelekezwa mjini Alexandria, Misri ambako Yanga SC itakuwa ikimenyana na wapinzani wao wa kihistoria kwenye michuaano ya Afrika, Al Ahly. Mchezo huo wa marudiano hatua ya 16 Bora unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa jeshi wa Borg El Arab kuanzia Saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Na katika mchezo huo, Yanga inatakiwa kushinda ugenini au kutoa …