Wenger Aingiwa na Wasiwasi Juu ya Mwenendo wa Arsenal

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ameanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. Anasema wasiwasi zaidi unatokana na hatari ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 19. The Gunners walipoteza nafasi ya kupanda hadi nambari tatu kwenye msimamoli baada ya kutoka sare tasa na …

Klabu Bingwa Ulaya Kuendelea Leo, Manchester City Kumkosa Yaya Toure

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya Nusu fainali inaendelea tena leo ambapo Manchester City watamenyana na Real Madrid. Manchester City wataikaribisha Real Madrid katika Mechi hiyo huku wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Kiungo wao kutoka Ivory Coast, Yaya Toure. Katika mchezo mwingine Atletico Madrid na Bayern Munchen watakukutana kesho jumatano Jijini Madrid katika Mechi ya Kwanza ya …

Yanga SC kufanya Uchaguzi Mkuu Juni 5

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam. Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu ya Young Africans utakuwa …

Leicester City Mwendo Mdundo, Arsenal Yapotezwa

Ligi kuu ya Uingereza imeendekea leo kwa michezo miwili ambapo Katika mchezo wa kwanza The Gunners wameambulia pointi moja baada ya kumaliza mchezo bila ya kufungana dhidi ya Sunderland Katika mchezo mwingine Leicester City wameendeleza juhudi za kusaka taji la ligi hiyo baada ya kuilaza Swansea mabao 4-0. Mabao ya Leicester yamefungwa na Riyad Mahrez (10), Jose Leonardo Ulloa (30) …

Yanga Vs Coastal Union Pambano Lavunjika, Azam Yatinga Fainali

Azam imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kufuatia ushindi wa penati 5-3 dhidi ya Mwadui FC baada ya timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2. Mechi hiyo ilibidi kuongezewa dakika 30 baada ya zile dakika 90 za kawaida kumalizika huku timu zote zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1. Azam walianza kufunga goli …

Manchester United Yatinga Fainali FA Kwa Mbinde

Klabu ya Manchester United Imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya FA baada ya kuisambaratisha timu ya Everton katika mchezo wa nusu uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley. Magoli ya Man United yamefungwa na marouane Fellain dakika ya 34 na dakika ya 90 Anthon Martial akifunga la pili, huku lile Everton likipatikana baada ya Beki wa Man U Chriss Smailling …