RAIS wa TFF, Leodegar Tenga kesho atafunga kozi ya ukocha kwa ajili ya kupata leseni za daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyofanyika kuanzia Novemba 7 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Dar es Salaam na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura ni kuwa shughuli za ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 30 utafanyika …
20 waitwa kuunda timu ya Taifa ya Vijana
KOCHA Mkuu wa timu za Taifa za vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Taifa kwa vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kitakachoshiriki michuano ya umri huo ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA). Michuano hiyo itafanyika Gaborone, Botswana kuanzia Desemba 1-10 mwaka huu ikishirikisha timu za mataifa 11 wanachama …
TFF yawataja waliochaguliwa kuongoza soka Mara
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limeweka wazi majina ya viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), baada ya uchaguzi ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya. Akitaja viongozi hao leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema katika uchaguzi huo uliendeshwa na …
Wachezaji 28 waitwa Kilimanjaro Stars
Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji inatakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu. Wachezaji walioteuliwa leo ni pamoja na Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari …
SBL yaalika wadau kuunga mkono udhamini michezo
Na Mwandishi Wetu KAMPUNI wadhamini wakuu wa Kombe la Tusker Chalenji, Serengeti Breweries Ltd (SBL), kupitia kinywaji chake cha bia ya Tusker, imewataka wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia juhudi za kukuza michezo nchini kwa kudhamini michezo. Changamoto hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi za TFF kuhusiana na mashindano ya …
Namibia yaingia michuano ya Chalenji
Na Mwandishi Wetu NAMIBIA itashiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Novemba 25 mwaka huu ikiwa timu mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa. Akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam leo Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodger Tenga amesema Namibia inaingia moja kwa moja katika kundi A ambalo lina mabingwa watetezi Tanzania Bara, …