Na Mwandishi Wetu WADHAMINI wakuu wa Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) wamewataka Watanzania na wadau wa Soka nchini kutokata tamaa a timu za Tanzania kupoteza mechi zao za kwanza. Kauli hiyo imetolewa leo katika Uwanja wa Taifa na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Phraim Mafuru alipokuwa akizungumza na wana habari mara …
Tanzania yaanza vibaya Tusker Chalenji
Na Mwandishi Wetu MECHI ya Mashindano ya Tusker Chalenji kati ya Timu ya Tanzania, Kilimanjaro Stars na timu ya Rwanda imemalizika muda mfupi huku vijana wa Rwanda wakiibuka vinara wa mchezo huo. Rwanda imefanikiwa kushinda mchezo huo kwa kuilaza Kilimanjaro Stars 1-0, goli lililofungwa katika dakika 22 kipindi cha kwanza cha mchezo na nahodha wa Rwanda, Kalekezi Olivier. Kilimanjaro ambao …
Bingwa Uhai Cup kujulikana leo Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu BINGWA wa Michuano ya Kombe la Uhai anatarajiwa kujulikana leo baada ya mechi ya fainali ya michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Kombe hilo (Uhai Cup) kwa klabu za Ligi Kuu kufanyika leo majira ya saa 3.00 asubuhi kwenye Uwanja wa Karume. Awali fainali hiyo kati ya Simba ambayo iliingia hatua hiyo kwa …
Watanzania wawili kucheza ligi daraja la pili Sweden
WACHEZAJI wawili wa Kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya Ligi Daraja la Pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio(Trials). Kwa mujibu wa taarifa zaidi zinasema majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya 30 ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya Ligi Daraja la Pili, KonyaSpor (KIF). Habari hii imeletwa …
Tenga ashinda tena u-Wenyekiti CECAFA
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Tenga amechaguliwa leo (Novemba 24 mwaka huu) bila kupingwa baada ya mpinzani wake Fadoul Hussein wa Djibouti kutotokea kwenye uchaguzi. Kutokana na hali hiyo, mjumbe kutoka Uganda alitoa hoja …