Sita wafariki katika ajali ya basi la wachezaji-Togo.

Watu sita walifariki baada ya basi lililokua likisafirisha wachezaji wa klabu ya mpira wa miguu Etoile Filante kudondoka katika korongo na kushika moto. Ajali hiyo ilitokea umbali wa maili 100 kaskazini mwa mji mkuu Lome wakati wachezaji hao wanakwenda kupambana na Timu nyingine katika michuano ya Ligi ya Togo. Pamoja na maofisa sita waliofariki, wengine 25 wamelazwa katika hospitali kwa …

Liverpool na Manchester City hakuna mbabe.

Bao la kujifunga la Joleon Lescott lilifuta jitihada za awali za Vincent Kompany kufunga bao wakati Manchester City walipoongeza wigo wa pointi hadi tano wakiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England. Liverpool yatoka sare na Manchester City bao 1-1 Mario Balotelli alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za manjano katika kipindi …

Zanzibar yashindwa kutamba kwa Burundi

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Zanzibar, imeshindwa kutumia fursa ya kucheza nyumbani huku ikishangilia na idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu jijini Dar es Salaam. Zanzibar ambayo katika mchezo wake wa kwanza iliupoteza leo imeshindwa kutamba dhidi ya vijana wa Burundi baada ya kutoka sulu ya bila kufungana hadi dakika 90 zinamalizika. Akizungumza mara baada ya …

Zimbabwe yainyoa Djibouti Kombe la Tusker

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Zimbabwe leo mchana imefanikiwa kiibanjua timu ya Djibouti mabao 2-0, katika Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Zimbabwe katika mchezo huo walionekana kuwakamia vijana wa Djibouti hivyo kuwashambulia muda wote katika lango lao tangu dakika za mwanzo za mchezo huo. Vijana wa Zimbabwe walianza kufungua kitabu cha magoli katika dakika …

Arsenal presha juu kwa Fulham

Arsenal imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 1-1 na Fulham. Beki wa Arsenal Thomas Vermaelen alijifunga mwenyewe na kuipa Fulham bao la kuongoza katika dakika ya 65. Hata hivyo beki huyo alifuta makosa yake dakika nane baadaye kwa kusawazisha goli hilo kwa kupachika mpira wa kichwa kutokana na krosi iliyopigwa na Theo Walcott. Kipa wa …

Man U haina jipya kwa Newcastle

Manchester United imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Newcastle United. Sare hiyo imeifanya Newcastle iliyo katika nafasi ya tatu kuwa na pointi moja tu nyuma ya United iliyo nafasi ya pili nyuma ya United. Goli la Manchester United limefungwa na Javier Hernandez, huku goli ya Newcastle likifungwa na Demba Ba kwa mkwaju …