Emmanuel Macron Rais Mpya Taifa la Ufaransa

EMMANUEL Macron ameshinda Uchaguzi wa Urais wa Ufaransa. Matokeo yanaonesha Macron amemuacha kwa mbali mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa kujinyakulia asilimia 65 ya kura. Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha bendera. Akiwa na miaka 39, Macron anakuwa rais waumri mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza Ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya …

Kuwanasa Wauaji wa Albino Kunaitaji Mbinu za Kivita!

  KWA wakazi wa Kitongoji cha Kona Nne, Kijiji cha Ugembe II, Kata ya Mwakashanhala wilayani Nzega katika Mkoa wa Tabora, takriban kilometa 90 kutoka Nzega mjini, saa 3:00 ni usiku mkubwa na wengi wamelala baada ya shughuli za ujenzi wa taifa. Majira kama hayo, usiku wa Jumatatu, Juni 15, 2015 haukuwa na tofauti kubwa, isipokuwa giza lililotanda kutokana na mbalamwezi kuwa gizani. …

Jacob Zuma Awatumbua Mawaziri, Yumo Waziri wa Fedha

RAIS wa nchi ya Afrika Kusini, Jacob Zuma amewafukuza kazi mawaziri wake kadhaa akiwemo Waziri wa Fedha, Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio wanaotajwa kulazimika kwake kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri. Taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu ya nchi ya Afrika Kusini zinaeleza kuwa tayari, Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Fedha wa taifa hilo …

Balozi Marmo Amvisha Cheo Kanali Joseph Bakari wa JWTZ

  KATIKA hali ambayo haijazoeleka Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo nchini Ujerumani alimvisha Cheo Kanali Joseph Bakari aliyepandishwa Cheo hivi karibuni kutoka Luteni kanali. Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na  ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii …

Al-Shabab Washambulia Kambi ya Majeshi ya Kenya nchini Somalia

Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia. Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya. “Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango …

AU Kujadili Madai ya Haki za Ardhi kwa Wanawake Barani Afrika

      Meneja wa Haki za Wanawake kutoka Actionaid Tanzania, Scholastica Haule akionesha nakala yenye madai hayo kwa vyombo vya habari walipokutana kumpongeza Mjumbe mwakilishi kutoka nchi za Afrika Mashariki wa Baraza la Wanawake wa Vijijini, Florah Mathias kupata nafasi hiyo.