JIMBO moja nchini Nigeria limetangaza hali ya hatari kutokana na uhaba mkubwa wa nyanya. Jimbo hilo la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, limechukua hatua hiyo baada ya wadudu waharibifu wajulikanao kama Tomato Leaf Miner au Tuta Absoluta kuharibu nyanya mashambani. Kamishna wa Kilimo katika jimbo hilo Daniel Manzo Maigar amesema wadudu hao wameharibu 80% ya nyanya katika jimbo hilo. Amesema wakulima …
Kampuni za Uchimbaji Zatunisha Mapato Serikalini – TEITI
Na Mwandishi Maalumu MAPATO ya Serikali ya Tanzania yanayotokana na shughuli za uchimbaji yameongezeka kwa asilimia 28 katika kipindi cha mwaka 2013/14, kwa mujibu wa ripoti ya sita ya asasi nayoshughulika na biashara hiyo – Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) – kwa kipindi kinachoishia Juni 30, mwaka jana. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo iliandaliwa na BDO East Africa …
VIJUE VIWANGO VYA TOZO KWA WATUMIAJI DARAJA LA NYERERE
VIWANGO VYA TOZO KWA WATUMIAJI WA DARAJA LA NYERERE Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Wadau wa Sekta ya Usafiri imeidhinisha viwango vya Tozo kwa watumiaji wa Daraja la Kigamboni vitakavyoanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosi tarehe 14 Mei, 2016. S/NA AINA KIWANGO CHA TOZO 1 WATEMBEA KWA …
Tozo Daraja la Nyerere Kuanza Rasmi Jumamosi
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza rasmi tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyererejijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, amesema kuwa tozo hizo zitaanza kutumika rasmi Jumamosi wiki hii na zitahusisha vyombo vyote vya usafiri. “Hakikisheni mnazifahamu tozo zote zitazotumika …
NMB Yatoa Ofa ya Uwekezaji kwa Wananchi…!
BENKI ya NMB imetoa ofa ya hati fungani kwa wananchi wanaotaka kuwekeza kwa muda wa miaka mitatu katika mtaji wa benki hiyo, huku wakijipatia faida ya asilimia 13 ya fedha waliyowekeza kwa kila miezi sita. Ofa hiyo imefunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker. Alisema …
Rais Magufuli Atoa Onyo kwa Wafanyabiashara Wanaoficha Sukari
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara wote walioficha sukari katika maghala yao, kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuinyang’anya sukari hiyo na kuisambaza kwa wananchi bure. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 06 Mei, 2016 katika mikoa ya Singida na Manyara wakati akizungumza na wananchi …