Sekondari Kongwa Zapangiwa Wastani wa Ufaulu…!

Na Mathias Canal, Dodoma MKUU wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi amewaagiza wakuu wa shule za Sekondari zote za Wilaya hiyo kuhakikisha wanafikia ufaulu kuanzia asilimia 41% ili kuakisi hali ya ukuaji wa ufaulu nchini na kupata wanafunzi waliopikwa vyema darasani ili kuwa na wasomi wenye weledi pasina mashaka. Dc Ndejembi amesema kuwa hatarajii kusikia shule mojawapo Wilayani humo …

Ujenzi wa Daraja la Salenda Kuanza Juni Mwaka Ujao

Ujenzi wa Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 …

Madereva 10 wa Tanzania Waliotekwa na Waasi Congo DRC Wawasili Nchini

     Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Balozi …

Mkemia wa Serikali Kupima Matumizi ya Vilevi kwa Madereva

  Na Beatrice Lyimo, Maelezo – Dar es Salaam WAKALA ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekusudia kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi kwa madereva wanaosafirisha abiria na mizigo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani nchini. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele alipokuwa akifungua mafunzo …

TTCL Yasaidia Tani 30 za Saruji kwa Waathirika wa Tetemeko Kagera

        Na Mwandishi Wetu, Kagera KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), imekabidhi msaada wa tani 30 za mifuko ya saruji zenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kusaidia jitihada za Serikali za kukarabati miundombinu mbalimbali iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera. Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim …

Waziri Amuagiza Mkuu wa Wilaya Kuziba Nyufa za Tetemeko la Ardhi

  Na Beatrice Lyimo, MAELEZO WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kufanya ukarabati wa haraka wa kuziba nyufa zilizotokea katika taasisi za Serikali zilizoathirika kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea hivi karibuni Mkoani humo. Waziri Mhagama aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua taasisi mbalimbali za Serikali …