DFID Kuijenga Upya Sekondari ya Ihungo Kagera kwa Bil 6.3

Na Frank Shija, Maelezo MSAADA wa Shilingi bilioni 6.3 umetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyo haribika baada ya kuathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba mkoani Kagera. Hayo yabainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habari …

LHRC Yasherekea Miaka 21 na Watoto Yatima Kurasini Dar

  Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.     Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya …

Waziri Lukuvi Afuta Hati 3 Eneo la Makaburi Kinyerezi

  Jonas Kamaleki, MAELEZO WAKAZI wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria. Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo …

Makonda na Wenzake Wawili Watumbuliwa

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha. Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri …

India Yachangia Maafa ya Kagera sh Milioni 545

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 27 Septemba, 2016 amepokea msaada wa Shilingi Milioni 545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, 2016. Hundi ya fedha hizo imekabidhiwa leo Ikulu Jijini …

Wadau wa Sekta ya Barabara na Reli Watakiwa Kuchangamkia Fursa

  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara kushirikiana na Serikali katika kuchangamkia fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta hiyo hapa nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba wa wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema kwa sasa …