MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. Makonda ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL …
Tanzania na Cuba Kuendeleza Ushirikiano…!
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mh. Salvador Valdes Mesa wakati alipokutana naye Ikuu leo kwa mazungumzo ambapo wamezungumzia jitihada za Serikali hizi mbili ya Cuba na Tanzania katika kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.(PICHA …
Mradi wa Mbogamboga wa Wanawake Manispaa ya Morogoro…!
Mkurugenzi wa mawasiliano wa taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika, Anna Salado (kulia), akipakua mboga zilizopikwa kiasili na kuungwa kwa nazi wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea mradi wa ukaushaji wa mboga na matunda wa wanawake wa Kata ya Mzinga mkoani Morogoro hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Milikieli Mansweat Mahiku. Mratibu wa mradi wa Green Voices kutoka taasisi ya Mfuko …
NMB Yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja…!
<strong>MKURUGENZI</strong> Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker leo ameadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kukutana na baadhi ya wateja wa Tawi la NMB Msasani huku akisikiliza maoni ya wateja katika hafla iliyoambatana na kunywa pamoja chai na wateja hao pamoja na wageni wengine waliohudhuria shughuli hiyo. Alisema katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa …
Tume ya Uchaguzi Kuendelea na Mafunzo kwa Wapiga Kura
Na Aron Msigwa – NEC Dar es salaam MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura kote nchini ili kuwajengea wananchi uelewa sahihi juu majukumu ya Tume na chaguzi zinazofanyika nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Lubuva amesema baadhi ya wananchi wamekuwa …
Makamu wa Rais Aongoza Kampeni ya Upandaji Miti Dar
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN leo tarehe 1-Oct-2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam. Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini …