Tabata Kimanga na Kero ya Takataka Barabarani

 Takataka zikiwa kando ya barabara. Mwendesha bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.   Na Dotto Mwaibale   WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.   Akizungumza na mtandao …

Rais Magufuli Achachamaa, Awataka ‘Vigogo’ Kurejesha Posho za Mwenge

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe Taarifa iliyotolewa leo tarehe …

NEC Yawataka Wanafunzi Sekondari Kuwa Mabalozi Elimu ya Mpiga Kura

  Na Aron Msigwa – NEC, Bariadi TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wanafunzi wa shule za Sekondari waliopatiwa elimu ya Mpiga Kura katika maeneo mbalimbali nchini kuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu waliyoipata kwa jamii inayowazunguka. Wito huo umetolewa na Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Fausta Mahenge wakati akitoa elimu ya mpiga …

Profesa Mbarawa Awabana Madereva wa Malori ya Mchanga na Kokoto

    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wa malori ya mchanga na kokoto watakaobainika kutofuata sheria za ubebaji wa bidhaa hiyo na hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara. Waziri Mbarawa …

Baraza la Watoto Mkoani Mwanza Lataka Fursa Sawa kwa Watoto

  Mwenyekiti wa Baraza la Watoto mkoani Mwanza, Paulina Mashauri, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambayo Jijini Mwanza yamefanyika hii leo Oktoba 11, katika Uwanja wa Furahisha na kuwashirikisha watoto kutoka shule na taasisi mbalimbali. Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali Wanafunzi wasichana wakiigiza michezo na maigizo mbalimbali Kulikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo …

TAMWA Yaanza Kutoa Mafunzo Uandishi Habari za Usalama Barabarani

        MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. Alisema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa …