
IKIWA ni siku kadhaa baada ya kuibuka tuhuma za wanajeshi kupora vitu kadhaa katika uvamizi wa maduka ya Westgate, Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya wamewaonya waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika sakata hilo lililosababisha mauaji, kujeruhi na uharibifu mkubwa.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa za wanajeshi kufanya uporaji katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi hao waliokuwa wamewateka nyara watu waliokuweme ndani ya jumba hilo kubwa la maduka.
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema kuwa waandishi hawapaswi kutoa habari au kuchochea propaganda, au kuwachochea Wakenya wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya waandishi wa habari wamehojiwa na polisi leo kuhusiana na sakata hilo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa waandishi wa habari zilionesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na mifuko ya plastiki iliyoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai hayo na kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo wanajeshi na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari Kenya vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa operesheni yao kutokana na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri kutoka kwa wakuu wa usalama.
-BBC

Maji ya kunywa inachukuliwa na mfuko wa plastic utakunywa namna gani? wanajeshi wa kenya wasitudanganye au kutisha wananchi wao ni waporaji wameiba vitu mbalimbali ikiwemo dhahabu,almasi na fedha nyingi sana alafu wakaangusha paa la juu iliyokuwa sehemu ya kuegesha magari na wasitoe jambo lolote la vitisho kwa wakenya kwa ujumla opereshen yenu dhidi ya magaidi imefeli mpaka mkawaua askari wa GSU kwa hiyo ilikuwa nyinyi wenyewe kwa wenyewe na magaidi wote wametoka na hawako nchini pamoja na msaada mliopata kutoka kwa wauwaji wakubwa wayahudi na marekani dawa ni kidogo sana tokeni nchi ya watu wenyewe watatatua matatizo yao.