Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua juu Taarifa na vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jina mojawapo la mtumishi aliyegushi cheti katika taarifa hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
One thought on “Rais Magufuli na Taarifa ya Vyeti Feki Chimwaga, Dodoma”
Hatua aliyoichukua JPM ni mzuri sana na inapaswa kupongezwa, Maana kuwa na mfanyakazi aliyefoji chetu katika utumizi wa umma ni janga kubwa sana, Maana utendaji wake hautakuwa wenye ufanisi na weledi Maana hana taaluma husika. Ila hili fyagio litaathiri wengi sana, watoto wanaosoma, wafanya Kazi wa ndani, wenye Nyumba za kupanga, vinyozi, Bodaboda, wazee vijijini. Nk. Hats hivyo nchi haiwezi kuendelea kama tutakuwa na wafanya Kazi vihiyo. Uwekwe utaratibu madhubuti kubaini vihiyo mapema..Mungu ibariki Tanzania