Rais Kenyatta Ateuwa Mawaziri Wanne wa Serikali Yake

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda Serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne ikiwa ni mchakato wa kuunda Serikali yake mpya. Mawaziri wanne walioteuliwa ni pamoja na Dk. Fred Okeng’o Matiangi ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.

Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.

Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.

-BBC

Related Post

One thought on “Rais Kenyatta Ateuwa Mawaziri Wanne wa Serikali Yake

  1. 18 ministers! now this is a guy who has the interest of the tax-payer at heart. sisi tuna 56 na wanatoroka bungeni huku walipa kodi wakiendelea kubeba mzigo wa kuwalipa hata posho za makalio

Comments are closed.