Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. Nikamsamehe.
Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe
wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito.
Kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu. kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe…na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate. sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
Nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? Hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena.. nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa…sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo:
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile.
Mpeni msaada wa mawazo mdau huyu jamani……….
Chanzo : UDAKU SPECIALLY


Nakusikitikia, kwa nn umeamua kujibu mapigo? Umeanzaje, au na wewe ulufanya siri kubwa sana? Kama umeamua na hujali kitakachofuata, ebu mueleze mumeo halafu urudi utueleze yatakayokukuta maana umesema upo tayari kwa lolote, haipendezi, mbele za watu na mbele ya Mungu wako pia.
Usijibu matatizo kwa upanga maana waweza kukurudia na kukukata wewe mwenyewe
Hamna haja ya kuanziasha mashindano. Mume kama huyo ni kuachana nae tu, maana kwa mtiririko wa matukio inaonyesha si mtu wa kubadilika.
Shosti maamuzi uliyoamua si sahihi na unatuzalilisha wanawake wenzio, muungwana hashindani kwa mabaya, kama yeye anatabia kama hiyo ni vizuri ukatafuta namna ya kumsaidia ili aachanae na hiyo tabia, waeleze wazee ili mupate msaada au muonane na viongozi wa dini. ubaya haulipi kwa ubaya kumbuka kuwa wewe una taifa zima la vijana wa baadae wannee wanaohitaji malezi ya hali ya juu katika awamu hii ya utandawazi na facebook. pls mpenziiiiiiiiiii achana na hiyo dhana angali future ya watoto, pia mkumbuke maradhi ya zinaa ni mengi mtakuja kuwafanya watoto wawe chokoraa. kwa mwenye akili zake timamu kukulaumu lazima coz uamuzi wako sio sahihi
UAMUZI ULIOCHUKUA SIO MZURI KWANI UNACHOTAKIWA NI KUTULIA ILI UWEZE KULEA WTT WAKO KWANI MARADHI NI MENGI AMBAYO YANAWEZA PELEKEA KIFO NA MATESO KWA WTT, MHM NI KUTOJIHUSISHA KIMAPENZI NA MUMEO KWAN INAONEKANA CMWAMINIFU TENA ANAWEZA KUKULETEA MAGONJWA.
MIDHARI NYUMBA IPO TULIA NA WATOTO WAKO ACHA ARANDE
Huyo mwanaume ni kiwembe, lakini na wewe ukianza Kwenda nje utaonekana kicheche. Unatakiwa umbanie uchi, ili asije akakuletea Maradhi, halafu unafanya utaratibu wa kuachana nae kimoja. Ukijifanya bado unampenda sana, utakuja umia.
Poa tu mwendo mdundo,ilonalo ni jibu. just uamuz.
pole kwa yaliokukuta, lakini kwa uamuzi wako hauko sahihi, utakua unajikomoa mwenyewe, uctafute faraja au amani kwa binadam amani na faraja vinapatikana kwa Mungu..,embu mwambie Mungu amshughulikie huyo mume wako uone kama hata badilika.,,
Wanaume wengi hu-cheat. So you are not alone. Usifuate anayofanya. Mwisho wa siku utajidharaurisha kwa jamii and you will feel guilt kwa maisha yako yote. Kumbuka watoto wanakua. Wakijua mama naye ni kama baba itakuwaje? kuwa na msimamo na maisha yako kama ilivyokuwa mwanzo. Hata huyo utakaye-cheat naye atakuwa na wengine pia- so chain itaendelea. Mumeo ni lile kundi la wanaume wasiopitwa na siketi ambao ni wengi mno. Tatizo ni kuwa hawajifahamu jinsi walivyo, kuwa wanasisimka kwa kuona, wengi wao wakiona wanamatamanio yasiyoisha. waweza kutamani miguu, kucha, nywele, midomo, pua, macho, makalio, hips, vidole, kifua, sauti, etc. list ni ndefu sana ambayo si rahisi kwa binadamu wa kawaida kuwa navyo vyote na vikabadilika badilika kama yeye anavyohitaji. Ni ufinyu wa mawazo. Funga na sugua magoti, Mwenyezi Mungu atakupa faraja na maisha yatasonga mbele. mwache ahangaike na dunia. Hata vitabu vitakatifu vinasema ” aziniye na mwanamke ni mjinga”. so mchukulie kama mjinga fulani.
the best thing u can only do is b patient and take care of ur kids. Dawa ya moto ni moto, mpango ya kando is the only medicine 4 him.