

Mtoto Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.

Tuseme nini manaake mpaka mtu anateketea akiwa hai je kuna serikali nchi hiyo?Ningependa huyo waziri wa afya wa nchi hiyo maanake haoni hata aibu mtoto mdogo anateketea akiwa hai hata wakati ule wa ukoloni mzungu angekuna kichwa kwa uchungu na huruma lakini mwafrika ndio anafikiria kupeleka mboga kwa mkewe angalia tu sura ya huyo mtoto alafu uniambie kuna serikali nchi hiyo na huduma nzuri ya afya kwa kusema kweli nchi imekufa.