Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jerry Silaa kushoto akishiriki kuimba nyimbo za kuhamasisha katika mkutano wa kampeni kumnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa Jimbo la Kalenga uliofanyika kwenye Kijiji cha Ibumila kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga na Anthony Mavunde kutoka Dodoma wakijumuika pamoja.
Kada wa chama cha Mapinduzi Bw. Fredrick Mwakalebela akipigia debe mgombea ubunge wa Jimbo la Lalenga kupitia CCM, Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Lalenga kupitia CCM, Bw. Godfrey Mgimwa akivishwa mgorole na wazee wa kimila kama ishara ya heshima mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.