Matokeo kidato cha nne yatangazwa, 3,303 wafutiwa matokeo

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA), Dk. Jocye Ndalichako

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka 2011/2012, ambapo pamoja na mambo mengine kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2.6.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Jocye Ndalichako alisema licha ya kupanda kwa kiwango cha ufaulu, tatizo la udanganyifu kwa wanafunzi limeongezeka na julma ya wanafunzi 3,303 wamefutiwa matokeo.

Dk. Ndalichako alisema NECTA imefikia hatua ya kuwafutia matokeo watahiniwa hao baada ya kukutwa na majibu katika nguo na wengine kuandika matusi katika vitabu vyao vya kujibia maswali.

Amesema Baraza la Mitihani linaangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua wanafunzi wanaoandika lugha za matusi katika vitabu vya majibu ambapo baraza litawasiliana na mwanasheria mkuu wa Serikali kuona ni hatua gani zitakazo chukuliwa.

Aidha baraza la mitihani Tanzania limetoa onyo kali kwa wamiliki wote wa vituo na shule ambazo zimejihusisha na udanganyifu pamoja na wasimamizi waliobainika katika kuwaandikia watahiniwa. Amesema orodha ya wahusika itapelekwa kwa waajiri wao ili wachukuliwe hatua stahiki. Pata matokeo zaidi kwa kubofya link hapo chini; http://196.44.162.14/necta2011/olevel.htm
http://www.necta.go.tz/results.html

Related Post

6 thoughts on “Matokeo kidato cha nne yatangazwa, 3,303 wafutiwa matokeo

    1. Mimi sina iman kabisa hata hao walio ongoza kitaifa ,maana Elimu TANZANIA imeguzwa kuwa biashara zaidi ,wamiliki wa shule hufanya kila wawezalo ili taasisi hizo zi zidi kupata wateja,wazili ,wizara husika amekili wazi kuwa udanganyifu umefanyika ikiwemo kuingia na dafutali za notes kwenye vyumba vya mitiani ,hivyo walio ongoza wame ongoza kundi la wajinga ,Usauli wangu wafikapo huko shulen(i A-LEVER) wafinyiwe Interview upya hata alie ongoza
      KWA UJENZI WA TAIFA.

      1. Its about ten years ago, my heart is in peace less, this is because of inconvenience that happened many years a go of stilling LUPILA SECO SCHOOL LABORATORY INSTRUMENT BY CERTAIN TEACHER. My cry is to my young daughter and son. What is paining me why no any action taken to this stilers so as to be a lesson to others who are there to jeopardize Government effort. I`m still crying in daily basis! GOVERNMENT STOP ME NOW.

  1. NINA FURAHA KUBWA PERFECT MINISTER UMELUDI ,WADOGO ZANGU NAWA SHAULI KAZENI BUTI KUPATA CHETI CHENYE SAHIHI YA Hon, NDALICHAKO SIO KAZI LELEMAMA, JIPANGENI SAWASAWA

  2. Huu sio wakati wa kutembea ,niwakati wa kukimbia kwasababu wezentu huko magharibi wana kimbia ,uamzi ulio fanywa na waziri wa Elimu kuhusu wanafunzi wa UDON ni sahii ,ili tuweze kufika pale walipo fika wenzetu , tuna hitaji strong decision

Comments are closed.