

SHULE ya Sekondari ya Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi shuleni. Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi. Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho wanahudhuria masomo yao.







