Lowassa pamoja na mgombea mwenza Haji Duni Haji ukielekea ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu za kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.

Mwalimu akizungumza.

Na Mwandishi Wetu, Dar
MSAFARA wa mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa ambaye pia anaungwa mkono na vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD umejumuisha umati mkubwa wa wafuasi wa vyama hivyo jambo ambalo limelazimisha baadhi ya maeneo shughuli kusimama kwa muda na watu kujaa barabarani kutazama umani huo.
Hali hii imeweka historia mpya kwa jijini Dar es Salaam kwa msafara mmoja kukusanya idadi kubwa ya wananchi kwa pamoja huku baadhi ya maeneo shughuli zikisimama na kushuhudia hali hiyo hasa barabaza za Uhuru kutokea Buguruni yalipo makao makuu ya CUF, kuja hadi makutano ya barabara ya Uhuru na Bibi Titi na baadaye barabara ya Ohio kwenda hadi zilipo ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC).
Msafara huo wa pikipiki, magari na watembea kwa miguu ambao ulikuwa maalumu kwa Lowassa na mgombea mwenza Haji Duni Haji ulilazimu baadhi ya ofisi na maduka ya wafanyabiashara yaliyopo kando ya barabara msafara ulipopita kufungwa kwa muda ili kupisha msafara kupita kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza.
Msafara huo ulioanza saa tatu maeneo ya Buguruni uliendelea hadi katikati ya jiji zilipo ofisi za NEC na baadaye kurudi na barabara ya Ali Hassan Mwinyi, barabara ya Kinondoni na kutokezea Barabara ya Kawawa hadi uwanja wa Biafra ambao ulitumika kwa dharura baada ya eneo la Ofisi za Chadema kushindwa kupokea idadi ya watu waliokuwa katika msafara huo.
Awali ilitangazwa baada ya Lowassa kuchukua fomu angerudi hadi Makao Makuu ya Chadema kinondoni kwa ajili ya kuwashukuru wananchi jambo ambalo lilishindikana kutokana na ufinyu wa nafasi hivyo kulazimika kuwaelekeza wananchi waende uwanja wa Biafra. “…Ndugu wananchi tunaomba radhi mgombea wetu na msafara wake hawata kuja hapa (Makao Makuu ya Chadema Dar) kutokana na ufinyu wa nafasi tumeelekeza waende kwanza uwanja wa Biafra akawatawanye wananchi ili arudi hapa kumalizia shughuli,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu akizungumza na umati uliokuwepo eneo la Makao makuu ya ofisi za Chadema Dar.
Aliwaomba wananchi waliopo pale wasiondoke kwenda Biafra maana tayari uwanja umejaa hivyo wabaki pale ili baada ya kuwaaga wananchi Viwanja vya Biafra Lowassa atarejea tena Makao Makuu ya Chadema na kuzungumza na wanachama na wananchi waliojitokeza kumpokea eneo hilo. Wakiwa makutano ya Barabara ya Biti Titi, Ali Hassan Mwinyi na Ohio (mataa) baadhi ya viongozi wa vyama walilazimika kushuka kwenye magari yao na kutembea kwa miguu kuelekea ofisi za NEC baada ya watu, magari na pikipiki kufurika jirani na ofisi za tume hivyo magari mengine kushindwa kufika eneo hilo.
Akiwahutumia wananchi na wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA Lowassa aliwashukuru kwa kujitokeza kumsindikiza kuchukua fomu na kuwaomba wajitokeze kwa wingi huo huo siku ya kupiga kura Oktoba 25, 2015 katika vituo vya kupigia kura. Aliwaomba kutunza kwa umakini shahada zao za kupigia kura ili zizije kutoweka na hivyo wao kukosa sifa ya kupiga kura.
Alisema akifanikiwa kuingia madarakani ataunda Serikali rafiki wa mama lishe, wamachinga, bodaboda na vijana kwa ujumla ili kuweza kutatua changamoto za vijana katika maisha yao. Alisema Serikali iliyopo madarakani imeshindwa kupambana na umasikini wa raia jamba ambalo aliwataka wawaache wengine waifanye kazi hiyo.
Kwa upande wake mgombea mwenza, Haji Duni aliwaomba Watanzania wakubali kuwaamini wao na kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi ili waende kupambana na umasikini wa nchi ulioshindwa kuondolewa na CCM tangu uhuru. Alisema wanakwenda ikulu kuwatumikia Watanzania bila kujali itikadi zao. “…Hatuendi ikulu kujenga makanisa, kujenda misikiti wala kutafuta utajiri tunakwenda ikulu kupambana na umasikini wa Watanzania hasa wa hali ya chini ambao wametelekezwa na Serikali ya CCM,” alisema Duni akizungumza na wanachama na raia waliojitokeza.
Msafara wa Lowassa uliongozana na mgombea mwenza, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, viongozi wa juu wa vyama vinavyounda UKAWA pamoja na viongozi mbalimbali wa Chadema.