
Na Shaaban Mdoe na Lilian Joel, Arusha
UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu.
Mnyika alisema kufuatia kitendo hicho Mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia ‘drip’ aliyohisi ilikua na lengo la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa.
Mnyika alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha wakati akisubiri wabunge wanne wa chama chake pamoja na wafuasi wao waliohusika na mkusanyiko usio halali katika viwanja vya Soweto jijini Arusha jana.
Kwa mujibu wa Mnyika, kufuatia hali hiyo Nassari aliamua kutoroka usiku wa kuamkia leo na kutokomea pasipojulikana ili kujinusuru maisha yake na kwamba Chadema baada ya kupata taarifa hiyo imeamua kumtafutia mbunge huyo hospitali nyingine itakayomtibu kwa gharama za chama hicho.
Pia Mnyika alisema mbali na tukio hilo pia polisi kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali hiyo wamekuwa wakiwaruhusu majeruhi wa tukio la mlipuko wa bomu kwenda majumbani kwao kabla ya kupata nafuu ikiwa ni hatua ya kupoteza ushahidi wa tukio hilo.
“Nassari amelazimika kutoroka hospitalini jana usiku baada ya kutundikiwa ‘drip’ na watu tunaowajua ni maofisa usalama iliyokua na lengo la kummaliza ambayo aliitoa na kisha kuanza kupiga yowe katika korido ili kuomba msaada na alifanikiwa kutoroka sasa tutamtibu sisi wenyewe,” alisema Mnyika.
Mnyika aliwataja maofisa usalama hao kuwa, John Ngowi na Flugence Mark ambao wamekuwepo hospitalini hapo kwa siku kadhaa wakitoa huduma kwa majeruhi wa ajali ya mlipuko wa bomu lililosababisha vifo vya watu nne na kujeruhi zaidi ya 70.
Akijibu tuhuma hizo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Paul Kisanga alisema si kweli kwamba mbunge huyo alitoroka hospitalini hapo bali alipewa ruhusa katika hali ya kawaida baada ya kuonekana hana tatizo lolote linalomsumbua tangu kufika hospitalini hapo.
Dk. Kisanga alisema mbunge huyo alipewa ruhusa hiyo siku ya Jumanne majira ya saa 9.30 alasiri bila kuwa na malalamiko yoyote kuhusu kutaka kudhuriwa na madaktari anaowadai kuwa ni maofisa usalama waliotumwa na serikali.
Aidha alisema mbunge huyo katika kuondoka kwake hakua na masharti yoyote kuwa anahitaji kupata uhamisho wa kwenda katika hospitali nyingine yoyote kwa matibabu zaidi kwakua hata alipotembelewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alimweleza wazi kuwa afya yake imeimarika.
“Mimi namshangaa Nassari kama kweli ametoa tuhuma hizo sisi tumemruhusu baada ya kusema kuwa anaona afya yake imeimarika na hata mbele ya Waziri Mkuu aliyasema hayo na kwanini hakuyasema hayo kwa uongozi wa hospitali kabla, huu ni uzushi,” alisema Dk. Kisanga.
Wakati huo huo, Kaimu mganga huyo alisema mtoto Fahali Jamali (7) aliyekua melazwa katika chumba cha ungalizi maalumu (ICU) tangu siku ya tukio amefariki dunia jana saa saba mchana kufutia hali yake kuwa mbaya zaidi. Dk. Kisanga alisema marehemu Fahali alifariki dunia kufuatia majeraha makubwa kichwani yaliyosababisha matundu matatu aliyoyapata kutokana na kulipukiwa na bomu siku ya tukio hilo.
Aidha aliongeza kuwa mara baada ya marehemu huyo kufariki mwili wake ulichukuliwa na Jeshi la Polisi pamoja na mzazi wake hadi katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya taratibu za maziko kufanyika.

DAWA YA WAONGO NI KUWAUMBUA TU KAMA HIVI!!!!
Mi wakati mwingine huwa siwaelewi wana siasa wa nchi hii!! Yaani sasa kazi yao kubwa imekuwa ni kuteka hisia za wananchi eti kwa kusudi la kuonekana wao wema dhidi ya upande mwingine. Hili linanikera sana mimi, kwa sababu sasa badala ya kutumia muda kujadili masuala ya maendeleo ya Mtanzania, wamekuwa wakitumia fedha za wananchi na rasilimali za nchi kuendekeza mijadala na marumbano ya kisiasa, huku maslahi ya vyama vyao yakiwekwa mbele kuliko maisha ya Mtanzania anayeishi katika maisha magumu! Kiukweli, hadi sasa, mimi sijaona mwana siasa ambaye kwa dhati anataka kulifaidia TAIFA. Ikiwa yupo, itakuwa ni yule ambaye anawaza, Nikijifanyia hiki, na kile, na familia yangu, na jamaa zangu, kisha nitafafanya hivi,…. kwa ajili ya TAIFA. Maneno ya mtunzi wa kitabu, The Beautiful ones are Not yet born” bado yanaendelea kuwa na ukweli hasa kwa siasa za Tanzania. Nitakuambia, kwa nini hoja yangu ina mantiki. Hembu kama si uchu wa madaraka walio nao wana siasa, wakae chini kwa upendo wakati wanapotaka kusimamisha mgombea yeyote, kisha mtu asipige kampeni ya kuchaguliwa, bali wanachama wenyewe wawe wanapendekeza kuwa fulani anastahili kututumikia katika nafasi fulani, wasifu wake utolewe, kisha watu wapige kura kumchagua, siyo yeye atumie pesa nyingi kwenda kujitangaza mwenyewe kuwa anafaa na kuwalaghai watu. Nina ujasiri wa kusema kuwa wana siasa walio wengi kama si wote, huwa wanatathimini keki iliyo pale juu, ndo mate yanawadondoka kama mbwa anavyofanya wakati anapoona mnofu kama Avogadro alivyowafanyia majaribio. Kinachofuata baada ya mate kuwatoka ni kuazimia kufanya kila liwezekanalo ili mradi tu afike kwenye keki na kuitafuna. Mfano mzuri uko huku vyuoni katika elimu ya juu, ambako kuna vijana wengi tena wanaojifanya kuwa wana uchungu na rasilimali za nchi. Pindi inapofika uchaguzi wa serikali za wanavyuo, utakuta mtu anaanza mapema kampeni za kugombea, huku akiwa ameandaa fedha nyingi ama kwa kukopa, ama kwa kulimbikiza ili mradi tu aweze kuteka kundi kubwa la watu wakati wa uchaguzi. Sasa mi huwa najiuliza, utakuta mtu katoka jasho na misuli, ati anataka Uraisi ili akatumikie wana chuo, kazi haina mshahara ila yeye anawekeza pesa nyingi kwenye mradi huo, hadi za kukopa. Atapataje pesa za kurudisha, mimi na wewe hatujui! Sasa itokee ameukosa uraisi, weeee!! movement zitaanzishwa hapo, oh wamenichakachua, mar hivi!! Kumbe mradi aliowekeza pesa nyingi umempiga hasara. Sasa njoo kwa yule aliyekitata kiti, wanafunzi tutachangia mfuko wa serikali kwa milioni zaidi ya mia moja (1000 Mill.), chuo kitatoa ruzuku zaidi ya Milioni mia, lakini mwisho wa uongozi wake, hakuna hata senti inayobaki, hakuna mchanganuo wa jinsi pesa ilivyotumika, hakuna kitu cha kuonekana kilichofanyika kwa pesa hizo zaidi ya kuona watu wakinunua magari, wakijenga nyumba n.k. Hii inatuambia nini kuhusu mstakabali wa TAIFA letu hasa kuhusiana na Uaminifu wa wale wanaoendelea kupikwa kisiasa ili wawe viongozi wa kesho? Na ni hawa hawa ndo ambao kesho baada ya kumaliza vyuo tunawakuta kwenye majukwaa ya kisiasa eti wakisema kuwa wao ndo wanastahili kushika dola, wapi! huu ni unafiki na ulaghai!! Wamekwishafanya mazoezi ya kuiba keki ya Taifa tangu wako huko katika jumuia ndogo sasa wanataka kuexercise wizi wao katika ngazi za juu zaidi. Na hii haijalishi kuwa mtu yuko katika chama gani cha siasa, ama ni upinzani, au ni chama tawala, wote ni sawa. Na hapa ndo nataka kuhitimisha kuwa, There is no correlation between the name of political party and the political candidate in terms of quality of leadership and behaviour. A good behaviour is a result is an outcome of the long nurturing process that takes place in the society from which an individual comes from. Kwa hiyo napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kuwa, tunapomtathimini mtu kuhusu ubora wake katika nafasi za uongozi, yatupaswa tuwe na uwanja mpana wa kufanyia tathimini usiofungwa na mipaka ya kichama na siasa.