
Na Joachim Mushi, Rombo KUFANYA vizuri kwa thamani ya fedha ya Kenya (Kshs) tofauti na ile ya Tanzania (Tshs) kumechangia kwa namna moja kuiathiri Wilaya ya Rombo maeneo ya mpakani mwa Kenya na Tanzania kitaaluma kwa kile baadhi ya wanafunzi wa sekondari kuacha shule na kwenda kufanya vibarua vijiji vya jirani. Uchunguzi uliofanywa na mwandishi [...]

Na Joachim Mushi, Rombo SHUGHULI za biashara zinazoendeshwa maeneo kadhaa ya mpakani mwa Tanzania na Kenya katika Wilaya ya Rombo zimeathiri maendeleo ya elimu hasa kwa shule za sekondari zilizopo pembezoni mwa maeneo hayo kwa kile wanafunzi kujiingiza katika biashara hizo. Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni wilayani hapa na mwandishi wa habari hizi umebaini baadhi ya [...]

Na Thehabari.com, Rombo HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au kujeruhi wakazi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa, Mkurugenzi [...]

Na Joachim Mushi, Handeni “KESI nyingi za tuhuma za kubaka na mimba kwa wanafunzi zinazotufikia zinashindwa kufikia hukumu maana mashahidi wanashindwa kuthibitisha pasipo shaka…nyingi zinaharibika sababu hawataki kusema ukweli, hivi karibuni nililazimika kuwaweka ndani wawili (mashahidi) kwa kuwa wanadanganya. Unakuta maelezo aliyotoa polisi ni mengine na akifika huku anageuka,” anasema Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi wa [...]

Na Joachim Mushi, Handeni MWANAFUNZI wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo, Mwenjuma Magalu (16) amejikuta akibeba mzigo wa kulea familia baada ya familia hiyo kutelekezwa na babayake. Mwanafunzi huyo anayeishi katika Kijini cha Msasa amejikuta katika hali hiyo ngumu baada ya mama yake mzazi, Hadija Magalu kufariki dunia ambaye ndiye aliyekuwa akiihudumia familia [...]

Na Joachim Mushi, Handeni “BAADA ya kumaliza darasa la saba nilichaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, lakini sikufanikiwa kuendelea na elimu hiyo kutokana na uwezo wa mzazi wangu mmoja (mama) ambaye alishindwa kumudu gharama zilizokuwa zikihitajika kwa wakati…,”ndivyo anavyoanza kusimulia Mwenjuma Magalu akizungumza Kijijini Msasa, Wilaya ya Handeni. Magalu anasema furaha zote alizokuwa nazo mwaka [...]

RIPOTI ya viashiria vya Ukimwi nchini katika mwaka 2011/12 imeonyesha kuwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 23 na 24 wameambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 6.6, ikilinganishwa na wavulana wa umri huo ambao ni asilimia 2.8. Akisoma ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, (Tacaids), Dk [...]