Blogs Tanzania | News |  Michuzi ya Habari leo

 

Category archives for: Michezo

Afrika Kusini Kuamua Mechi ya Taifa Stars Vs Morocco

nembo ya shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the Atlas).   Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco kwenye Uwanja wa Grand kuanzia [...]

14 Kuumana Ligi ya Mabingwa Mikoa

Boniface Wambura Ofisa Habari TFF

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele. Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa [...]

Pambano la Yanga, Simba Laingiza Mil 500/-

PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-

PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.   Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 [...]

Yanga Yauwa Simba, Yaichapa 2-0 Uwanja wa Taifa

Mchezaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Simba Abdallah Seseme katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam imekamilisha mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kuibanjua Timu ya Simba magoli 2-0 bila kujali machungu ilionayo timu hiyo kwa kukosa ubingwa wa ligi hiyo kwa mwaka huu. Mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu [...]

Pazia Ligi Kuu Vodacom Kufungwa Mei 18

Boni Wambura

LIGI KUU ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu (2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14 kupambana katika viwanja saba tofauti. Mechi zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa [...]

Taifa Stars Yajiondoa Michuano ya COSAFA

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah

TANZANIA (Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.   Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba [...]

Kocha Kim Awataja Wachezaji 26 Watakao Ivaa Morocco

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen Mei 16 mwaka huu ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.   Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku [...]

 

 

Log in |

 

Google+