
Maandamano makubwa kupinga mauaji Songea yanafanyika, polisi watawanya kwa risasi za moto, wawili wadaiwa kufa
Na Mwandishi wa dev.kisakuzi.com Songea
TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata muda huu ni kwamba maandamano makubwa yanafanywa na Wananchi Wilaya ya Songea wakioinga matukio ya mauaji mfululizo yanayodaiwa kuhusishwa na imani za uchimbaji wa madini ya uraniamu eneo la Namtumbo.
Taarifa zaidi zinadai Jeshi la Polisi Wilayani Songea limewapiga risasi na kuwauwa waandamanaji wawili wakiwa wanajitahidi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakitokea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Songea kuelekea Hospitali ya Wilaya na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Hadi sasa watu wanaokadiriwa 14 wameuwawa kikatili na kuondolewa baadhi ya viungo vya sehemu za siri huku taarifa ambazo hazijathibitishwa zikidai vinatumika katika matambiko kwenye migodi ya Uraniamu huko Namtumbo. Tayari muandishi wa dev.kisakuzi.com (www.thehabari.com) Namtumbo yupo eneo la tukio na muda si mrefu tutawarushia picha za matukio na taarifa kamili za vurugu za maandamano hayo.
Hivi kwanini haya yanatokea? serikali yetu inasubiri mambo yaharibike ndiyo ianze kuuwa watu wasio na hatia? inasikitisha sana. Maisha ya mtanzania saahizi ni magumu sana, bado tunashambuliana wenyewe kwa wenyewe, kwanini serikali isikilize kero za wananchi?
NI JAMBO LA BUSARA SANA KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANANCHI KABLA HALI KAMA HII HAIJATOKEA. JAMANI MBONA TUNAIPOTEZA AMANI YETU?