Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarabu la 5 Star, kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati wakitokea mikoani kuja Dar es Salaam.
Inasemekana waliotambuliwa kufariki dunia mpaka sasa ni pamoja na Issa Kijoti, Hamisa Omary, Husna Mapande, omary Hashim, Nasor na Shaby Juma. Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinasema tayari miili ya marehemu hao imeondolewa eneo la ajali na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro.
Mdau mmoja wa masuala ya muziki amethibitisha kupatwa na ajali kwa wanamuziki hao, kwani amedai simu zao zinapigwa na kuita bila majibu kati ya kundi lililokuwa likisafiri katika gari hilo.
Inadaiwa jumla ya watu sita (6) wamefariki dunia katika ajali hiyo. Taarifa zaidi zitatolewa na The Habari kadri zitakavyotufikia, endelea kufuatilia.
Poleni ndugu wa wafiwa mungu alaze roho za mrehem mahali pema amen.
inasikitisha sana,nawapa pole wafiwa wote waliopoteza ndugu zao inauma,watanzania tumepata pigo kubwa kuwapoteza wanamuziki wakongwe na wapenzi wazuri mungu awalaze mahali pema peponi
Poleni sana , Ndugu na jamaa wa Ajali hiyo.
Inna Lilah Waina Ilahi rajiuun. poleni sana wana wa 5start. wao mbele sisi nyuma yao. tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu wapumzishwe maala pema peponi
jaman poleni sana ndugu zang wafiwa kazi ya mola haina makosa
Poleni watanzania
poleni sana wana wa 5 star kwa msiba mkubwa uliotokea Morogoro Waswahili wanasema apangacho Mwenyezimungu hakuna binadamu anaeweza kupangua Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi Amina