
MASHINDANO ya vipaji vya mpira ya ‘Guinness Football Challenge’ yamemalizika jana katika viwanja vya Leaders na kupatikana timu nane za watu wawili wawili kila timu ambao wanatarajia kupelekwa nchini Afrika Kusini kujiunga katika shule maalumu ya vipaji vya mpira wa miguu. Mashindano hayo ambayo yamezaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) chini ya kinywaji chao cha Guinness yalifanyika jana ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.


