
Na Mwandishi wetu
KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana jana jijini Dar es Salaam kimemteua Dk. Dalaly Peter Kafumu kuwa Mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Igunga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, CCM imekubaliana kufanya kampeni zake kwa kutumia helkopta ili kuyafikia maeneo yote ya wapiga kura.
Nape alisema kampeni hizo ambazo zinatarajiwa kuzinduliwa na rais mstaafu, Benjamin Mkapa muda utakapowadia, wamepanga kutumia helkopta kutokana na muda ufupi uliopo wa kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa CCM eneo hilo.
“Katika kipindi hicho cha kampeni Chama cha Mapinduzi kinakusudia kutumia helkopta ili kuyafikia maeneo yote ya Igunga kwa urahisi kwani muda wa kampeni ni mfupi. Hivyo kwa njia ya kawaida si rahisi kuyafikia maeneo yote kwa usafiri wa kawaida kwa kipindi hicho,” alisema Nape katika taarifa hiyo.
Nape alisema CCM katika kampeni hizo inatarajia kutumia kauli mbiu isemayo; ‘Tumethubutu, Tumeweza, Tunasonga mbele’
Nape! kutumia helkopta sio ujanja, bali inaonyesha ni kiasi gani mnaendelea kufisadi na kukejeli wanyonge. Suluhu ni kutengeneza miundombinu ya uhakika, ili kila sehemu ya nchi yetu iweze kufikika! Dar es salaam yenyewe foleni mpaka kwenye majumba ya watu…..sasa “tunasonga mbele” kuelekea wapi ? Kama bado kuna sehemu hazifikiki huko Igunga, je ni kitu gani basi mnachojivunia huko Igunga kwa miaka yote mliyoshikilia jimbo? Je hamuoni kama hii ni sababu ya msingi kwa wanachi wa Igunga kuwapiga chini?