
KAMPUNI ya vifaa vya kieletroniki  ya  Samsung  imezindua  kampeni  ya  kuweka  oda  kwabidhaa  yake  mpya  ya  Galaxy  Note 4  nchini  Tanzania, ikiwa  ni sehemu  ya  kushamirisha  uzinduzi  mkubwa  utakofuatia  wa bidhaa  inayosubiriwa  kwa  shauku  ya  Samsung Galaxy Note 4.  Kampeni hiyo itakayoendeshwa kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi14 Novemba 2014, inadhamiria kuwapa wateja wake wakudumu nafasi ya kujipatia bidhaa hiyo ya kisasa zaidi katikafamilia ya simu za kiganjani za Note.  Hali  kadhalika  kampeni itawawezesha  wateja 100  kujipatia zawadi ya Gear S  ambayo  ni saa  za  kisasa  za  Samsung  inayo tumika  sambamba  na  simu hiyo.
Wakati ulimwengu wa teknolojia ya simu za kiganjaniukipanuka zaidi na zaidi, kila mwaka kampuni ya Samsunghutoa bidhaa mpya ili kuwapa wateja wake uwanja mpana wakupata kumiliki na kutumia bidhaa zenye teknolojia ya kisasa nahali ya juu kuendana na mabadiliko daima ya teknolojia.
Katikamiongo iliyopita, bara la Afrika limekuwa kama mtazamaji kwamaendeleo ya teknolojia ya simu za viganjani zilizokuwazikianzishwa kwenye soko la kimataifa. Siku hizo za utazamajizimepitwa na wakati. Enzi  zile  mtu  kumiliki  simu  za  teknolojia ya  kisasa  ilikua  kwa  yule  aliyetoka  safari  ughaibuni  au  ndugu ametoka  ughaibuni  na  zawadi  ya  vifaa  hivyo,  leo  kampuni  za simu  zinatuletea  vifaa  hivi  vya  kisasa  mlangoni  kwetu.
Ongezeko  la  nguvu  za  nchi  za  kiafrika  katika  nyanja  mbalimbali  inahashiria  bara  la  Afrika  ni  soko  muhimu  kwa  nyakati hizi  kulinganisha  na  hapo  mwanzo.  Ukuaji  wa  mara  mbili  zaidi ya  bara la Asia,  soko  la  simu  za  kiganjani  la  Afrika  linaonyesha ukuaji  wa  kasi, tukio ambalo kampuni za simu ulimwengunihalijashindwa kulitambua.
Ikikatisha  mfumo  wa  kuzindua  bidhaa  mpya  katika  masoko  ya kimataifa  na  yaliyoendela  ya  barani  Ulaya, Marekani, Korea  ya Kusini  na  Asia,  Kampuni  ya  simu  za  mkononi  ya  Samsung katika  miaka  ya  karibuni  imekuwa  ikipeleka  bidhaa  zake  kwa soko  ya  ndani  Afika.
Gwiji  la  kampuni  za  simu  za  viganjani  la Samsung  limekuwa likizindua  bidhaa  zake  kadha  wa  kadha  za  kisasa  katika  nchi zilizoko  kusini  mwa  jangwa  la  Sahara,  ikiwemo  uzinduzi  mpya wake  wa  simu  yake  mpya  ya  Samsung  Galaxy Note 4.   Uzinduzihuo,  ambao  awali  ulifanyika  huko  Afrika  ya  Kusini,  unategemea kufanyika  nchini  Tanzania  katika  siku  za  usoni.
Katika  kusubiri  shamra  za  uzinduzi  wa  simu  hiyo  mpya inayotarajia  kufanyika  Novemba  14,  2014, Samsung  wanatoa nafasi  za  pekee  kwa  wateja  wake  wa  Tanzania  kuwa  wa  kwanza kununua  na  kumiliki  Samsung  Galaxy  Note  4  kupitia oda  hiyo.
Utoaji  wa  oda  hiyo  utafanywa  kwa  muda  wa  wiki  mbili  kuelekea kwenye  uzinduzi  utakaofanyika  jijini Dar es Salaam.  Oda  hizo zitawapa  pia  wateja  wapya  nafasi  kuwa  katika  mstari  wa  mbele wa  kumiliki  simu  hiyo  mashuhuri  inayo subiriwa  kwa  shauku kubwa  na  wadau.  Ili  kuweka  oda,  wateja  wanatakiwa  kufanyamambo 3.
Hatua  ya  kwanza:  Wajisajili  kwa  kujipatia  Galaxy  Note 4  katika  tovuti  www.galaxynote4.co.tz  au  kwa  kutembelea maduka  ya  wakala  yalioidhinishwa  na  Samsung  na  kuhakikisha wanatunza  kuponi  zao  za  oda.  Hatua  ya  pili:  Nunua  bidhaa  hiyoya Note 4  kutoka  katika  maduka  husika  siku  ya  Novemba  14, 2014  na  kutunza  receipt  ya  manunuzi.  Hatua ya tatu:  Baada  ya manunuzi  ya  bidhaa  husika,  mteja  anapaswa  kujiunga  na program  ya  E-warranty.  Kujiandikisha  kwa  ajili  oda  mwisho 5:59  usiku  wa  tarehe 14  Nov. 2014  wakati  kujiunga  na  E-warranty  wateja  wanabidi  kutuma  SMS  ya  IMEI  namba  ya  simu zao  za  Note  4  kwenda  15685  mfano  reg*123456789123445# kwenda  15685. IMEI  namba  inapatikana  katika  simu ilionunuliwa  katika  sehemu  ya  kuweka  battery  ama  kwa  kupiga *#06#.
Droo  ya  kushindania  zawadi  za  bidhaa  za Gear S za  Samsung itafanyika  kwa  tarehe itakayotajwa  baadae kwa  watejawatakaokuwa  wamekamilisha  hatua  zote tatu. Samsung itazawadia  wale  watakao ibuka  washindi  katika  droo hiyo  kwa Gear S  bidhaa ambayo  inatumika  sambamba  na  Note 4,  na ilikumuezesha  kila mtu kuwa mshindi  mwisho wa siku, watakaokuwa  hawajabahatika kujishindia  Gear S  watapata  kava  za  simuya note 4.
Gear S  ni vifaa  vya kisasa kutoka  Samsung iliyo kwenyemuundo  wa  saa ambayo inaleta uzoefu wa simu mkononi mwamteja.  Vifaa  hivyo  vyenye muundo wa saa ya mkononivinamuezesha mtu kupokea na kupiga simu, pamoja namawasiliano kutumia Bluetooth na intaneti ya 3G.
Simu mpya ya Galaxy Note 4 imetengenezwa  kwa fremu  ya chuma  iliyotengenezwa  kwa  teknolojia ya  kisasa.  Simu  hiyo yasaizi  ndogo  inakupa urahisi kuweka kwenye mfuko ikiwa nakioo kipana zaidi kutosha kuangalia muvi.  Kioo chakekinauwezo wa  kuonyesha picha zenye  muonekano  mzuri kinachosindikizwa  na kalamu ya kisasa  inayomwezesha  mtumiaji  kuandika  kwa  mfumo  wa  kidigitali.  Simu hii  inauwezo  wa  kuchaji  kuanzia asilimia 0 mpaka 50% kwa dakika 30. Kama  ilivyo  kwa  simu  aina ya Galaxy S5  simu  hii  pia  ina mfumo  wa  kutunza  chaji  ambao  unaruhusu  kuhifadhi  chaji kwa ajili  ya  matumizi  ya muhimu  ya  simu  pale chaji  inapoisha kabisa.
Bw. Mike Seo, Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania anasema, “Simu za mkononi zimekuwa zaulazima katika ulimwengu wa sasa, hivyo sio budi kwa makampuni ya simu za kiganjani kutambua mahitaji ya sokolake. Soko la Tanzania linaonyesha kukua kwa kasi kwa wanunuzi na watumiaji wa simu wenye hulka kadha wa kadha. Kutokana na ukweli huo, tunashauku ya kuwatengenezea wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya kisasa zaidi zitakazo wapa matokeo ya kipekee, na wateja wetu wategemee kupata hicho kutoka Samsung Galaxy Note 4 na sio kingine.”
Kutokana na ongezeko la uelewa wa wateja kuhusu umuhimu wa vifaa vya teknolojia
