Mgomo wa wauza petroli, dizeli waendelea Dar es Salaam

Mgomo wa wauza petroli, dizeli waendelea Dar es Salaam

Na Joachim Mushi

MGOMO wa kinyemela kwa wauzaji wa mafuta ya petroli na dizeli umeendelea jana mjini Dar es Salaam, ambapo umezua kero kubwa kwa wamiliki wa vyombo vya moto na wafanyabiashara wa usafirishaji abiria jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mtandao wa dev.kisakuzi.com vituo vingi vya kuuzia mafuta vilikuwa havitoi huduma yoyote kwa visingizio kwamba vimeishiwa bidhaa hiyo ya nishati. Wakati idadi kubwa ya vituo hivyo vikiwa vimefungwa kero ilikuwa pia kwa wauzaji wa baadhi ya vituo kama Big Bon na Oilcom vilivyokuwa vinaendelea kutoa huduma hiyo.

Vituo hivi vilielemewa na wateja ambao walikuwa wakishindwa kufuata utaratibu uliowekwa kiasi cha kuvutana kati ya wateja ambao walionesha hofu ya kukosa huduma hiyo katika sehemu hizo chache zilizokuwa zikitoa huduma.

Vituo hivi vililazimika kuweka kiwango maalumu cha kila mteja kununua kiasi kidogo cha mafuta ili kuhakikisha huduma inawafikia wengi, angalau kuondoa makali ya uhaba wa nishati hiyo kwa watumiaji wa vyombo vya moto.

Vituo vya Big Bon vilivyokuwa vikitoa huduma hiyo viliweka utaratibu wa kuuza mafuta yasiodhidi thamani ya sh. 20,000 kwa kila mteja aliyekuwa katika foleni za vituo hivyo ili kuhakikisha kila mmoja angalau anapata kiasi kidogo cha mafuta hayo.

Hata hivyo misululu ya magari na watu waliobeba galoni za kubebea mafuta ndizo zilizokuwa zikifurika katika vituo ambavyo, vilionekana kutofanya mgomo huo baridi. Wakati hali hiyo ya kero ya mafuta ikiendelea tayari Serikali imetihia kuwafungia wafanyabiashara ambao wanaonekana kuendeleza mgomo huo wa kuendelea kuuza mafuta mara baada ya Serikali kutangaza kushuka kwa bei hizo.

Zifuatazo ni pica mbalimbali zikionesha wananchi wakiwa kwenye foleni ya mafuta;

"Maji shida, mafuta shida duh! Ama kweli Dar kila kitu ni foleni.
'Magari yapange foleni, na sisi tupange foleni...haya ndo maisha bana.'

Related Post

5 thoughts on “Mgomo wa wauza petroli, dizeli waendelea Dar es Salaam

  1. itabidi serikali yetu ijipange vizuri kwa kuwa tatizo hili linaonekana linaota mizizi ila serikali inabidi iangalie suala jipya la kurudisha huduma ya kusafisha mafuta katika kiwanda chetu cha tiper ili iweze kuzibidi suala la bei ili tuondokane na adha hii kubwa na mivutano ya mara kwa mara na na wafanyabiashara wa mafuta.kwani hakuna anayekubali hasara katika biashara yake,serikali iangalie suala hili kwa kina.

  2. Huu ni upuuz nchi haiwezi kuendeshwa kijinga namna hii serikali yetu iko likizo ama vp hawa wanojiita viongozi wamefanya nn kunusuru hali hii,biashara zetu zimesimama umeme hamna maji hamna mafuta nayo hakuna inamaana tulale nyumban na wake zetu ama vp?LAZIMA NGELEJA NA TIMU YAKE WAJIUZULU SABABU WAMESHNDWA KAZI WATU WACHACHE HAWAWEZI KUYUMBISHA UCHUMI WA NCHI,RAIS ,WAZIRI MKUU WAMEKAA KIMYA HAWANA LA KUSEMA JE WANAWAOGOPA WAFANYA BIASHARA WA MAFUTA?THIS IS BULLSHIT……………!

  3. Raya hao serikali ndio waliouwa kiwanda cha Tiper ili wafanye biashara zao kwa uhuru na Tiper haiwezi kurudi kwa ukiritimba huu

  4. Na ho wanaoendesha Biashara ya Mafuta baadhi ya viongozi serikalini wana hisa zao unategemea watakwambia nini wewe mwenzangu mimi.

Comments are closed.