
IMEBAINIKA kuwa balozi za nchi za Ulaya zilizopo nchini Tanzania, zikiwemo
balozi za Ujerumani, Ubelgiji, Netherland na nyinginezo zimekuwa zikiweka vikwazo kwa baadhi ya raia wa Tanzania wanaohitaji pasi za kusafaria kwenda katika nchi za ulaya.
Taarifa zinasema licha ya baadhi ya Watanzania kutimiza masharti yote yanayohitajika katika kuomba pasi, lakini balozi hizo zimekuwa zikiwawekea vikwazo visivyo katika sheria za maombi ya pasi. “…Mfano Mtanzania anapo omba pasi ya ubalozini atapeleka barua ya mwaliko na bima, pamoja na taarifa ya benki (benk statment), barua ya kazini, nakala za mishahara. Heti bado maofisa balozi wanadai barua nyingine itoke kwa mwenyeji kuonesha uhusiano na mgeni Mtanzania! Kwa kweli hakuna uhusiano mzuri katika ya raia na maofisa wa visa wa balozi za EU nchini Tanzania,” kilieleza chanzo.
“…Kimsingi Watanzania wanapoomba pasi za Ulaya wanasumbuliwa sana hapa nchini. Serikali inaweza kuwa na uhusiano mzuri na balozi hizo lakini raia wa Tanzania hawathaminiwi kabisa na balozi za EU hapa Tanzania,” kilieleza chanzo.

Msione ajabu kwa mabalozi wa EU kuweka ngumu ukweli ni kwamba waafrika wengi kutoka bara hili lengo lao ni kukwepa maisha ngumu iliyoko Afrika na hata wanajitahidi wakifika huko wanajitahidi kuoa wanawake wa huko ili wapate hati ya kuishi nchini na ikiwezekana baada ya muda wanabadilisha uraia alafu anakuja kutembea akiwa mtu mwingine sio yule ulikuwa unamjua lakini hawajui hii ni hasara kubwa sana ,mimi nawashauri mabalozi waendelee hivyo hao sio wajinga uongo wetu imepita kiasi na ukiagalia kwa undani Waafrika wanaoishi ulaya maisha yao ni ya hali ya chini sana ukilinganisha na nyumbani haswa kuhusu uhuru walionayo nyumbani .