


ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo jana aliongoza ibada maalumu ya kutoa daraja la ‘comunio’ kwa takribani watoto 54 wa Parokia ya Mtakatifu Joseph ya jijini Dar es Salaam.
Misa hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Paroko, Padri Joseph Masenge ilifanyika katika Kanisa Kuu la St. Joseph na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la jijini Dar es Salaam.






